Futa akaunti yako ya Kitab au data
Data yako ni yako. Unaweza kufuta sehemu yake au kufuta akaunti yote wakati wowote, bila gharama.
Kwenye programu
Fungua Kitab uende Zaidi › Programu › Data (kwenye kompyuta: jina lako juu kulia › Data). Chagua Futa data zangu kufuta unachochagua, au Futa akaunti kuondoa kila kitu.
Kinachofutwa na kinachobaki
- Futa data zangu: aina unazochagua (miamala na bili, mikopo, mali na thamani halisi, malengo, ripoti na nakala) zinafutwa kwenye seva za Kitab mara moja. Akaunti, mpango na mipangilio vinabaki. Kwa kila kumbukumbu iliyofutwa tunabakiza alama tu isiyo na maudhui, ili vifaa vyako vingine vijue kuondoa nakala yao.
- Futa akaunti: baada ya siku 14, akaunti yako na kila kilichomo vinafutwa kabisa: wasifu (jina, barua pepe, simu), kila kumbukumbu uliyoweka, mipangilio, vifaa vilivyoingia, arifa na tokeni za push. Hakuna kinachobaki baada ya hapo.
- Barua pepe ambazo Kitab ilishakutumia zinabaki kwenye sanduku lako. Faili ulizohamisha na kuhifadhi zinabaki ulipozihifadhi.